×

Hakika Ruben: Mapenzi sasa ni kuvamia tu – Video

KATIKA kipindi cha ‘255 Front Page’ asubuhi ya leo Desemba 14, studio za +255 Global Radio ametutembelea mchekeshaji anayekuja kwa kasi nchini, Hakika Ruben, ambaye ana-trend kwa sasa katika mitandao ya kijamii na na  tulipiga naye stori masuala mbalimbali ya kazi yake hiyo ya uchekeshaji.

 

 

Ameonyesha kushangazwa na baadhi ya mabinti ambao wamekuwa wakitolewa out na wapenzi wao badala ya kuja wao wanakuja na rundo la marafiki zao.

 

“Ujue mapenzi ya siku hizi ni kama tunavamiana tu, hakuna miiko, mimi nikiingia kwenye uhusiano na wewe lazima tuwekeane mipaka pamoja  ni hakuna kuombana pesa, lakini hii ya kuja na rundo la marafiki zako, ipo siku mtaachwa peke yenu mlipe bili wenyewe.” amesema Reuben.

Akizungumzia namna alivyoacha kufanya mambo ya Injili licha ya kuwa na taaluma ya Saikolojia na Theolojia, anasema video iliyomtambulisha zaidi ni pale aliponunua simu mpya na kujirekodi gizani akisema kuwa anauza giza, jambo ambalo mara baada ya kuiposti marafiki zake walianza kumpigia simu wakimweleza kuwa kitendo alichokifanya kitamsababishia akamatwe.

 

“Tanzania tu ndiyo unaweza kuwa maarufu ghafla, lakini umaarufu huu huwa haudumu, kuna watu wanakuwa maarufu kwa sababu ya kulewa.  Je, baada ya hapo ili uendelee kuwa maarufu zaidi utalewa zaidi ama? Kwangu mimi ni rahisi kwa sababu ninachokifanya hakina shida na ninaweza kukiendeleza vizuri,” amesema Hakika.

 

Leave a Comment