
POLISI Mkoa wa Mbeya linamshikilia Rashid Kindole (21) mkazi wa Mkunywa–Madibira Wilaya ya Mbarali kwa tuhuma za kupatikana na mali za wizi baada ya kuvunja nyumba usiku na kuiba.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei, mtuhumiwa alikamatwa Desemba 20, 2020, huko Mkunya katika msako wa polisi maeneo mbalimbali mkoani Mbeya.
Baada ya kupekuliwa nyumbani kwake alikutwa na mali mbalimbali za wizi zikiwemo vyombo vya muziki, kamera na betri za sola.
Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika.
Pia polisi mkoani humo inamshikilia Saamoja Kanandi (30) mkazi wa Ndola, Mbalizi, kwa kukutwa na gramu 380 za bangi alizomakatwa nazo huko Mtaa wa Mshikamano, Usongwe,.
Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika.