×

Shigongo Atua Maisome: Msiogope, Ni Pesa Zenu – Video

MBUNGE wa Buchosa, Mhe. Eric Shigongo, ameendelea na ziara katika maeneo tofauti ndani ya jimbo lake akitatua kero na kuwaelimisha wananchi juu ya miradi ya maendeleo na umuhimu wa kuifuatilia kwa karibu ambapo mapema jana Jumatatu, Januari 4, 2020, alifanya ziara yake katika Kisiwa cha Maisome.

Shigongo amewashukuru wananchi wa Kata ya Maisome kwa kumchagua kwa kura nyingi za ‘ndiyo’ na kuwa mwakilishi wao Bungeni na kusema kuwa wananchi wanatakiwa kuwa na uchungu na maendeleo yao ili waweze kufanya kazi kwa bidii na kujitolea kuleta maendeleo kwenye vijiji na kata yao ya Maisome.

 

Aidha,  amewasisitiza wananchi wa kata hiyo kuungana na kuwa kitu kimoja, jambo ambalo litaharakisha maendeleo katika maeneo yao.

Shigongo yupo jimboni kwake akifanya ziara na mikutano na wananchi wake ili kutatua kero zinazowakabili pamoja na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali na ile inayofanywa na wananchi wenyewe katika jimbo hilo.

Leave a Comment