×

Rekodi za Platinum zaipa jeuri Simba SC

REKODI mbaya waliyonayo timu ya FC Platinum katika michezo ya ugenini ya michuano ya kimataifa, inawafanya Simba watembee kifua mbele kuelekea mchezo wao wa marudiano.

Simba wanatarajiwa kuwa wenyeji wa FC Platinum katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo mchezo huo utachezwa kesho Jumatano kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.

Simba itaingia katika mchezo huo ikiwa nyuma kwa bao 1-0 lililofungwa na winga Perfect Chikwende katika mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza uliochezwa jijini Harare, Zimbabwe.

Rekodi za michezo tisa ya nyuma ya FC Platinum wakiwa ugenini inaonyesha kuwa wamepoteza michezo mitano, wakitoa sare michezo miwili na kushinda michezo miwili pekee jambo ambalo linawapa nafasi kubwa Simba kuibuka na ushindi kwa mujibu wa rekodi.

Platinum katika michezo hiyo tisa ya ugenini walipoteza dhidi ya Esperance 2-0, Horoya 2-0, Al Hilal 2-1, Al Ahly 2-0, Etoile Sahel 2-0 huku wakitoka sare dhidi ya Orlando Pirates 2-2 na Nyasa 0-0 na wakishinda dhidi ya UD Songo 4-2 na Costa do Sol 1-2.

 

MARCO MZUMBE, Dar es Salaam

Leave a Comment