×

JPM Aiomba China Mambo Matatu “Wanajua Hatuna Corona” – Video

Rais Dkt. John Magufuli leo Ijumaa, Januari 8, 2021, amempongeza Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi kwa kutovaa barakoa alipokuwa katika mkutano wa kusaini Mkataba wa kujenga Reli ya kisasa.

 

Magufuli amesema, Tanzania ni salama na katika kuthibitisha hilo, alikwenda kumpa mkono kabla ya kwenda kupiga picha ya pamoja na kupata chakula cha mchana.

 

“Ninampongeza sana Mhe. Wang Yi, anajua Tanzania hatuna Corona, ndiyo maana hakuvaa hata yale mabarakoa na mimi kwa kumthibitishia nakwenda kumshika mkono twende tukale chakula pamoja.

 

“Rais Xi Jinping nimemuomba watusaidie katika miradi mikubwa mitatu kule Njombe, nimemuomba watujengee KM 48 kule Zanzibar, nimemuomba watusamehe madeni yetu tuliyokuwa tumekopa, likiwemo lile tulilolibeba wakati tunajenga reli ya TAZARA.

 

“Kuna deni pia la nyumba za maaskari wetu la Dola Mil. 137, deni lingine ni la kiwanda cha Urafika Dola Milioni 15, wakatufutie tu sababu nchi ya China ni rafiki yetu na ni nchi tajiri na Mh. Waziri amesema atalifikisha hili ombi.

 

“China ni nchi tajiri na sisi tuna mazao mengi tunayoweza kuyapeleka China na ndiyo maana katika zawadi zangu nimetoa korosho, majani na Kahawa nikiamini kuwa wachina wakila tu nusu kilo ya korosho zetu maana yake watakuwa wanakula Tani Mil 750,” amesema Magufuli.

 

Leave a Comment