
Charity Group Tabora wameuanza mwaka kwa kuungana na kituo cha kulelea watu wenye mahitaji maalum cha Sisters of Charity kilochopo Tabora Mjini, ambapo walihusika katika kwa kuwapatia mahitaji mbalimbali ya shule na nyumbani.
Tukio hilo lililotokea hivi karibuni liliambatana na mkutano mkuu wa kwanza wa Charity Group.

Akizungumzia kuhusu mchakato huo, Uliofanyika Tabora Mjini kinapopatikana kituo cha kulelea watu wenye uhitaji maalum mwenyekiti wa kikundi hicho, ndugu Fundi Kassim Fundi aliwashukuru wahisani na wanachama wote wa Charity kwa moyo waliouonyesha wa upendo na mshikamano.
Aidha, Fundi Kassim aliiasa jamii kufanya matendo ya huruma ili kuleta mahusiano mazuri katika jamii.
Kikundi hicho kinapatikana mkoani Tabora, kinaundwa na Watendaji wa Kata, Vijiji na Mitaa Mkoa wa Tabora.
Kituo hicho kinaitwa SISTERS OF CHARITY na kinamilikiwa na masista wa Roman Catholic Jimbo Kuu Tabora.
