×

Bad News: Fisi Waua Watoto Wawili Geita

WATOTO wawili wamefariki dunia na watu wanne kunusurika kifo baada ya kuvamiwa na kushambuliwa na kundi la fisi ambao wamekuwa wakiingia mara kwa mara vijijini, wakati wakitoka shambani wilayani Nyang’hwale mkoani Geita.

 

 

Baadhi ya viongozi wa kijiji hicho  wamesema matukio ya fisi kuvamia kaya za watu yamekuwa yakijitokeza mara nyingi hali inayopelekea wananchi kuishi kwa mashaka kwa kuhofia uhai wao.

 

 

“Hii hali ipo wiki mbili zilizopita hapo bupamba aliliwa mtoto wa mika kama nanae hivi na fisi usiku akamalizwa kabisa, yametokea matukio mawili moa nyaghamila na moja hapa izingwa, hukun lilishambuliwa watu wazima,” amesema Mtemi Saleh Nzera Kiongozi wa Kimila.

 

“Jana nilipata habari kuna mtoto kangatwa na fisi akiwa anatoa mahindi ya kwenda kupika chakula cha jioni ilikuwa majira ya saa 11 jioni akawa maejeruhiwa na yuko hospitalai anaendelea na matibabau, kwa hiyo hii hali inazidi kutodhoofisha katika mipango maendeleo,” amesema Kafola Vicent Mwenyekiti wa Kitongoji Butalanda.

 

 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Mariam Chaurembo amekiri uwepo wa kundi la fisi wanowashambulia watoto na kusema kuwa tayari wadau wanaohusika na wanyamapori washawasili wilayanai hapo kwa ajili ya kuwawinda.

 

 

Tayari wameshakamata fisi sita na wameruhusu wanakijiji kuwawinda fisi hao ili kuuwawa kutokana na kukithiri kwa matukio hayo. Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Wilson Shimo amesema wameshatoa tahadhari kwa wananchi kuwatunza watoto hususan nyakati za jioni na asubuhi wasiwe wanatembea wenyewe.

 

Leave a Comment