×

Mama Mzazi wa Ronaldinho Afariki Dunia

MAMA mzazi wa nyota wa zamani wa Barcelona Ronaldo de Assis Moreira, maarufu kama Ronaldinho Gaucho, Dona Miguelina amefariki dunia jana Jumapili akiwa na umri wa miaka 71.

 

Kwa mujibu wa Ronaldinho mnamo mwezi Desemba mwaka jana Miguelina aliripotiwa kupata virusi vya corona na kulazwa hospitali, katika Mji wa Porto Alegre Brazil.

 

Licha ya Gaucho mwenyewe kutoweka wazi chanzo cha kifo cha mama yake mitandao mikubwa ya soka imeripoti kuwa ugonjwa wa Corona ndio uliokatisha uhai wake.

 

Ronalhinho kupitia akaunti yake ya Twitter amethibitisha kutokea kwa msiba huo.

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:
⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8​
⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave a Comment