×

Madaktari Waonya Dalili Mpya za Corona

LICHA ya dalili za awali zinazotambulika tangu wimbi la kwanza, pia kuna dalili nyingine zinazogunduliwa na madaktari hivi karibuni, ambazo zinahitaji uangalifu.

 

 

Madaktari nchini India wanaamini kuwa baadhi ya dalili zinazidi kuongezeka katika visa vilivyoripotiwa tangu mwezi uliopita.

 

 

Vidonda kwenye mdomo na ulimi

Madaktari wanabainisha kuongezeka kwa idadi ya visa vinavyojitokeza na dalili kama vidonda kwenye mdomo na ulimi ambavyo huambatana na dalili nyingine kama homa , kikohozi na uchovu.

 

 

Uvimbe kwenye ngozi na vidole

Kuna visa mbalimbali ulimwenguni kote vya wagonjwa wa Corona kuwa na uvimbe kwenye ngozi na vidole vya mikono.

 

 

Harara na vinundu kwenye ngozi

Wataalam wa Afya wanabainisha kuwa harara inayoweza kudumu kwa masaa kadhaa ni moja ya dalili ya Corona katika siku za mwanzo, pia huweza kusalia hata baada ya kupona Corona

Leave a Comment