
Mufti Aboubakar Zuberi ametoa pole kwa Watanzania wote na walioguswa na kifo cha Rais Magufuli kilichotokea Machi 17, 2021.
Amesema kwa Maadili ya Dini ya Kiislamu marehemu anatakiwa kukumbukwa kwa mazuri. Hivyo, ametoa wito kwa Watanzania kukumbuka mazuri ya Rais Magufuli.
Aidha, ameomba kuendelea kuomba dua ili atakayechukua nafasi ya Rais Magufuli ajaaliwe ‘tawfiq’ katika Uongozi.