
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella ametoa rai kwa Watoto na Wazee kufuatilia shughuli za kumuaga aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Dkt. John Magufuli kupitia Runinga.
Mwili wa Dkt. Magufuli unatarajiwa kuagwa Mwanza kesho Machi 24, 2021 katika Uwanja wa CCM Kirumba ukitokea Zanzibar.
Amesema, “Tuombe tena Wazazi, na hili sio katazo ni ushauri. Karibu Vituo vyote vya Televisheni vinaonesha matukio haya mubashara, basi watoto wa Shule za Msingi waachwe majumbani.”
Aidha, ametoa wito kwa Wazee wenye changamoto za kiafya nao kuangalia njia muafaka ya kufuatilia ikiwemo kupitia Runinga.