×

Yericko Nyerere Akwepa Jela Miaka Mitatu

Mfanyabiashara na mwanaharakati maarufu wa masuala ya kisiasa, Yericko Nyerere amelipa faini ya Sh5 milioni na kukwepa kifungo cha miaka mitatu jela.

 

Leo Jumanne Machi 23, 2021 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilimhukumu kada huyo wa Chadema kulipa faini hiyo au kwenda jela miaka mitatu baada ya kumtia hatia kwa kosa la kuchapisha maneno ya uchochezi katika mtandao wa kijamii wa Facebook, yenye lengo la uvunjifu wa amani.

 

Hukumu hiyo imetolewa na hakimu mkazi mkuu wa mahakama hiyo, Kassian Matembele. Nyerere anakabiliwa shtaka moja la kusambaza taarifa zinazodaiwa kuleta taharuki kwa watu kupitia akaunti yake ya kijamii ya Facebook kitendo anachodaiwa kukifanya Mei 28, 2017 mkoani Dar es Salaam.

 

 

Faini hiyo imelipwa leo jioni, Machi 23, 2021, baada wa wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendelea (Chadema), Kanda ya Pwani, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bavicha, John Pambalu kupitisha mchango wa kumchangia Yericko, baada kuhukumiwa na Mahakama hiyo, kulipa kiasi hicho cha fedha.

 

Leave a Comment