×

Real Madrid Yaitungua Barcelona 2-1

TIMU ya Real Madrid imepaa hadi kileleni mwa msimamo wa La Liga, na kuweka hai matumaini ya ubingwa baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Barcelona usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Alfredo Di Stéfano Jijini Madrid.

 

Mabao ya Real Madrid yamefungwa na Karim Benzema dakika ya 13 na Toni Kroos dakika ya 28, wakati la Barcelona lilifungwa na Oscar Mingueza dakika ya 60.

 

Kwa matokeo hayo , Real inafikisha pointi 66,  baada ya kushuka dimbani mara 30,sawa na Atletico Madrid yenye mechi moja mkononi na kupanda kileleni, wakati Barcelona inaangukia nafasi ya tatu ikibaki na pointi zake 65 baada ya mechi 30.

 

Barcelona imefungwa nyumbani na ugenini msimu kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2007 Real Madrid walipofanya hivyo

 

Leave a Comment