The House of Favourite Newspapers

Mume wa Malkia Kuzikwa Aprili 17, 2021

0

MAZISHI ya mume wa Malkia Elizabeth II wa Uingereza, Mwanamfalme Philip, yatafanyika wiki ijayo, Aprili 17, majira ya saa nane mchana, katika Kanisa la Mtakatifu George, Magharibi mwa London.

 

 

Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika Kasri la Buckingham, na mazishi hayo yataendeshwa kwa taratibu tofauti kutokana na vizuizi vya kupambana na janga la virusi vya corona.

 

 

Shughuli hiyo ya mazishi itahudhuriwa na watu 30 tu wa karibu na itarushwa moja kwa moja kupitia televisheni.

 

 

Mjukuu wake, Harry, ambaye kwa siku za karibuni, yeye na mkewe Meghan wamekuwa na mzozo na familia ya kifalme, anatarajiwa kuhudhuria katika mazishi hayo.

 

 

Bendera zitapepea nusu mlingoti kwenye majengo ya serikali hadi baada ya mazishi.

 

 

 

Mwanamfalme Phillip, aliyekuwa mume wa Malkia Elizabeth kwa kipindi cha miaka 73, amefariki akiwa na akiwa na umri wa miaka 99.

Leave A Reply