×

Kajala Mtegoni Sakata la Paula

DALILI mbalimbali zinaonesha kwamba kwenye ugomvi wa Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ na Rajabu Abdul ‘Harmonize’ kuna mkono wa bosi kubwa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ hivyo imeelezwa mwanamama Kajala Masanja anaweza kuingia mtegoni kwa bosi huyo wa Wasafi Classic Baby (WCB).


Chanzo makini kilicho karibu na mastaa hao, kimelitonya RISASI kuwa, baada ya Rayvanny kuvujisha meseji za Harmonize akimtongoza Kajala kwenye ukurasa wake wa Istagram, wapambe wa Diamond pamoja na uongozi mzima umekuwa upande wa Kajala.

 

“Yani kuanzia chawa wote kama kina Juma Lokole na wengineo wote wamemfanya Kajala kuwa rafiki wakati kabla hajaachana na Harmonize alikuwa adui yao.


Huu ni mtihani kwa shoga yangu Kajala maana anaweza kujikuta kwenye himaya ya Mondi bila kutegemea.

“Unajua Mondi kwa Kajala ni kama anarudi tu kwa mara ya pili kama ikitokea maana huko nyuma alishawahi kuwa naye sasa si unajua tena mtalaka hatongozwi? Asipokuwa makini anawezakujikuta amengia kwenye himaya ya Mondi,” kilisema chanzo hicho makini.

Vyanzo mbalimbali vimedai kuwa, safari ya matanuzi anayoifanya Kajala na mwanaye Paula pande za Dubai, ina mkono wa Mondi japo taarifa hiyo haijathibitishwa na Diamond wala uongozi wake.

Kajala ametupia picha mbalimbali zinazomuonesha akila bata Dubai huku ikielezwa analala kwenye moja ya hoteli za kifahari sana kwenye jiji hilo la starehe katika nchi ya Falme za Kirabu.

Leave a Comment