×

Waziri Mkuu Akasirishwa na Mwenendo Mbovu Mradi wa Mabasi ya Mwendokasi

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, leo amefanya ziara katika mradi wa mwendokasi kwa kuanzia na kituo cha Gerezani, Kariakoo na kubaini dosari nyingi katika uendeshaji wa mradi huo.

 

 

 

Akifanya ukaguzi katika mradi huo, Waziri Majaliwa amemhoji Mkurugenzi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Kasi (Dart), Mhandisi Ronald Lwakatare kwa nini mfumo wa ukusanyaji wa mapato unafanyika bila kutumia mifumo ya Tehama ambapo majibu yake yameonesha kutomridhisha Waziri Mkuu.

 

 

 

Pia Waziri Majaliwa amejionea mabasi yaliyoharibika ambayo yapo kwenye karakana kituoni hapo na kuhoji kwa nini hayafanyiwi marekebisho na badala yake, vipuri vyake vinatolewa na kufungwa kwenye mabasi mengine, ambapo majibu ya wataalam wa mradi huo yameonesha kutomridhisha.

 

Leave a Comment