
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema Ushindi wa CCM mwaka 2025 utaletwa kwa namna wana CCM watakavyotekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM huku akisisitiza kuwa Siasa si uadui hivyo kuviomba vyama vya siasa kutoa ushirikiano katika kuimarisha umoja uliopo.
Samia ameyasema hayo leo Ijumaa, Aprili 30,2021 wakati akishukuru baada Mkutano Mkuu Maalum wa CCM kumpitisha kuwa mwenyekiti mpya wa chama hicho kwa kupata kura zote 1862 za NDIYO.

Amesisitiza kuwa kazi ya kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi inaendelea kuhusu akibainisha kuwa hatawaangusha wanawake na watanzania kwa ujumla.
“Nawashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kunichagua kwa kura zote (100%) kuwa Mwenyekiti wa CCM. Nawaahidi utumishi uliotukuka na CCM imara ambayo inaongoza Serikali yetu ya Awamu ya Sita.

“Nitasimamia maadili na kanuni za chama ili kujenga chama imara. Niwatake viongozi wa CCM, kuacha kuwa sehemu ya kutengeneza migogoro, baina ya viongozi wa serikali na wananchi. Niwaombe wana CCM, kuhakikisha Ilani tuliyoinadi mwkaa jana, inatekelezeka. Ushindi wa 2025, utaletwa kwa namna tutakavyotekeleza ilani yetu.
‘Natambua changamoto mbalimbali ndani ya chama ikiwemo usafiri kwa viongozi wa ngazi za chini pamoja na maslahi duni ya watumishi wa chama, hivyo nitajitahidi kuzitatua kwa kushirikiana na nyinyi.

“Nafahamu kuwa nachukua jukumu la kukiongoza Chama hiki (CCM) kikiwa kina baadhi ya changamoto ikiwemo uhaba wa vitendea kazi, kuna baadhi ya Mikoa na Wilaya Viongozi hawana usafiri, changamoto nyingine ni maslahi duni kwa Watumishi wa Chama.
”Nitaweza kwanza kwasababu chama chetu kinaongozwa kwa Katiba, Kanuni na Taratibu, ambazo naahidi kuzifuata kikamilifu. Pili majukumu ya chama chetu yanatekelezwa na kila mmoja wetu kwenye ngazi mbalimbali hivyo jukumu hili sio langu peke yangu’.
”Niwahakikishie katika kipindi cha Uenyekiti wangu, nitashirikiana na nyinyi wote katika kuhakikisha tunasimamia misingi ya chama chetu, lakini pia kuendeleza utamaduni wa kujitathimini na kujisahihisha kwa lengo la kukijenga chama chetu.

”Mhe Mwenyekiti nakushukuru sana kwa kukubali kunipokea, kukubali kunisamehe na kuniruhusu mimi Lazaro Samwel Nyalandu, kurejea tena nyumbuni, kwa hakika hakuna furaha izidiyo furaha ya mtoto arejeaye nyumbani.”
“Niwatake viongozi wa CCM, kuacha kuwa sehemu ya kutengeneza migogoro, baina ya viongozi wa serikali na wananchi.

“Niwaombe wana CCM, kuhakikisha Ilani tuliyoinadi mwkaa jana, inatekelezeka. Ushindi wa 2025, utaletwa kwa namna tutakavyotekeleza ilani yetu. Nawashukuru viongozi wa chama chetu wa zama au awamu zote zilizopita kwa umakini wao katika kukiongoza chama chetu na kukifanya kuwa imara mpaka sasa.

“Niwashukuru sana wenzangu UWT na wanawake wote wa Tanzania bila kujali itikadi zao, tangu nimekuwa Rais, wanawake wote wameniunga mkono, nitaendelea kuwa nanyi na sitawaangusha. Nafahamu kuwa kuna malimbikizo ya madai ya stahiki zikiwemo za uhamisho na kustaafu, nawaahidi nitashirikiana na nyinyi kuzitatua changamoto zilizopo kwenye CCM nilizozitaja na ambazo sijazitaja,” amesema Samia.