×

Rais Samia: Tutapandisha Mishahara Mwakani – Video

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema jumla ya wafanyakazi zaidi ya 85,000 elfu hadi 91,000 watapanda vyeo mwaka ujao na kuajiri watumishi 40,000 katika Idara ya Elimu na Afya.

 

Ameyasema hayo kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Kitaifa leo Mei 1, 2021 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

 

“Ndugu zangu mimi ni mama, mama ni mlezi..Dai hili ni la msingi na la kweli. Mishahara haijaongezwa muda mrefu. Kutokana na mlipuko wa ugonjwa Corona uwezo wetu kiuchumi umepungua, imekuwa vigumu kwangu kuongeza mishahara lakini tutaboresha maslahi ya wafanyakazi,” amesema Rais Samia.

 

“Mishahara haijaongezwa kwa muda mrefu, Mimi binafsi natamani kuongeza mishahara mwaka huu ila kwasababu mbalimbali nimeshindwa, uchumi wa Tanzania umeshuka kutoka 6.9% hadi 4.7% kwasababu ya Corona, nawaahidi mwakani siku kama ya leo nitapandisha mishahara.

 

“Imekuwa ni vigumu kwangu na kwa sababu ndiyo nimeingia sijakaa vizuri, kuongeza mishahara mwaka huu. Kwa kutambua umuhimu wa wafanyakazi, tutaboresha maslahi kwa mwaka wa fedha 2021/22, kwa kupunguza viwango vya kodi ya mishara na mfumko wa bei.

 

“Mwakani siku kama ya leo nitakuja na package nzuri ya nyongeza za mishahara kwa watumishi, hivyo naagiza haraka kwa kuundwa kwa Bodi za Mishahara ili nifahamu kabisa tena mapema kuwa, mwakani napandisha mishahara kwa kiwango gani,” amesema Rais Samia.

 

Leave a Comment