
Sakata la Mbunge wa Tunduru, Condester Michael Sichalwe (CCM) kutolewa bungeni kipindi cha asubuhi kutokana na kuvaa mavazi yasiyoendana na maadili baada ya Mbunge wa Nyang’awele, kuomba mwongozo kwa Spika jambo lililopekea Mbunge huyo kutolewa nje ya Bunge na Spika ili akavaeavazi ya staha.
Jambo hilo limechukua sura mpya baada ya Mbunge wa Viti Maalum, Jackiline Ngonyani kuomba muongozo kwa Naibu Spika kuhusu jambo ilo.
“Namuomba mbunge Hussein Amar kuomba radhi kwa kumdanganya Spika kwa kuwa hoja ya Mbunge Hussein ilikuwa sio kweli kuwa mbunge Condester alikuwa amevaa mavazi yasiyostahili.
“Mhe. Naibu Spika kwa kweli nimeona kwenye mitandao kila mmoja akisema binti huyu ameonewa, kilichodaiwa na Mbunge mwenzetu sio kweli, alichofanya ni kumdhalilisha, aombe radhi kwa tukio la kumdhalilisha Mhe. Mbunge na kumdanganya Spika,” amesema Mbunge Ngonyani.
Naibu Spika alimpa nafasi pia Mbunge wa Nyasa, Eng. Stela Manyanya aliyeomba Mwongozo kuhusu jambo hilo; “Kwa kweli wanaume humu ndani wamekuwa wanatabia ya kudhalilisha wanawake na kuna wakati wanafikia kutaja ata viungo vya wanawake bila woga,” alisema Mbunge Manyanya.
Naibu Spika pia alimpa nafasi pia Mbunge Hussein Amar kuzungumza kuhusu jambo hilo ambaye ndiye aliyeliibua asubuhi, alisema;” Mhe. Naibu Spika, kwanza siombi radhi na kama inawezekana mbunge arudie mavazi yale, na mimi jambo la kuomba radhi siwezi kufanya hivyo,” alisema Hussein Amar.
Baada ya maelezo hayo, Naibu Spika alisema kutokana Na kanuni za Bunge, Spika anaweza kutoa majibu ya Muongozo alioombwa papo hapo au baadaye.