×

Vodacom Yashiriki Upandaji Miti Kuelekea Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani

Mkurugenzi Mkazi WWF, Dkt Aman Ngusaru(kulia), Mkurugenzi wa Vodacom Foundation (katikati) na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania Prof. Santos Silaya wakishiriki upandaji wa miti jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za kuelekea siku ya Mazingira Dunia. Vodacom Tanzania amekuwa ni mshirika mkubwa kwenye utunzaji wa mazingira ikiwa ni pamoja na upandaji wa miti ili kufanya Tanzania sehemu salama ya kuishi.
Zoezi la kupanda mti likiendelea katika eneo la Medeli jijini Dodoma.

Kampuni inayotoa huduma za simu ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na uongozi wa Mkoa wa Dodoma wameshirikiana kupanda mti katika eneo la Medeli jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za kuelekea siku ya kimataifa ya mazingira duniani. Utanzaji wa mazingira ni moja ya malengo ya Vodacom Tanzania Plc ya kuhakikisha kuwa dunia inakuwa mahali salama pa kuishi kwa kupanda miti na kuboresha mazingira kwa ujumla.

 

Picha kwa Hisani ya Vodacom Tanzania

Leave a Comment