×

Kim Jong-un Atoa Tamko Mapambano Mapya na Marekani!

UHASAMA unaozidi kukua kati ya Marekani na Korea Kaskazini ni kitisho kipya cha usalama wa dunia.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amesema, nchi yake inahitaji kujiandaa kikamilifu kwa mapambano na Marekani.

 

“Tunajiandaa kikamilifu kwa mapambano ili kulinda hadhi ya serikali yetu na masilahi yake kwa maendeleo huru.”

Bwana Kim amesema hayo alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa viongozi wakuu wa Chama cha Wafanyakazi katika mji mkuu wa Pyongyang wiki hii, shirika la habari la nchi hiyo KCNA limeripoti.

 

Uhusiano kati ya Kim na Rais wa Marekani Joe Biden umezorota ambapo kabla ya uchaguzi wa Marekani uliopita, Bwana Biden alimwita Kim “jambazi” na kuongeza kuwa nchi yake ni kitisho cha dunia.

 

Hata hivyo, Kim hakujibu matamshi Biden kwa maneno bali alifanya onesho kubwa la kijeshi lililokwenda sambamba na uzinduzi wa kombora jipya la masafa marefu.

 

Duru za kisiasa zinaonesha kuwa mgogoro wa mataifa hayo mawili yanayomiliki silaha za nyuklia unaweza kuitumbukiza dunia katika hali tete za kiusalama.

STORI NA RICH MANYOTA | GPL

Leave a Comment