The House of Favourite Newspapers

Yamoto, Kayumba wapo tayari kukinukisha Dar Live

0

YAMOTO-BAND-2STORI: ANDREW CARLOS
MAMBO yameiva! Bendi funika bovu Bongo, Yamoto na Mshindi wa Bongo Star Search (BSS 2015), Kayumba Juma wanatarajia kukinukisha ile mbaya ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live, Mbagala- Zakhem jijini Dar, Desemba 19, mwaka huu.

KAYUMBA (1)kizungumza na Ijumaa Wikienda, mratibu wa shoo hiyo, Mohamed Seif ‘Mudy K’ lisema kuwa mbali na kumtambulisha Kayumba atakayefanya shoo kwa mara ya kwanza siku hiyo, pia Yamoto wataachia ngoma yao mpya baada ya Cheza kwa Madoido ijulikanayo kama Imo.

“Kutakuwa na sapraizi kibao ambapo Baby J kutoka Zanzibar kwa mara ya kwanza atatambulisha wimbo mpya, familia yote ya Mkubwa na Wanawe itahamia Dar Live,” alisema Mudy K na kusisitiza kuwa kiingilio kitakuwa buku 10,000 tu.

Leave A Reply