×

Mwambusi: Yanga SC Wabadilishe Kikosi Leo

ALIYEKUWA Kocha mkuu wa Yanga SC, Juma Mwambusi ameweka wazi kuwa katika mchezo wa leo timu ya Yanga inabidi iamke kwa kutatua changamoto zote uwanjani ili kupata matokeo yatakayowapa ubingwa kwenye michuano ya Kombe la Kagame, ikibidi wabadili kikosi.

 

Ikiwa na alama mbili tu kwenye michuano ya Kombe la Kagame, Yanga itaenda kukutana na kinara wa Kundi A, Express FC wakiwa na alama nne leo jioni, kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.


Akizungumza na Championi Jumamosi, Mwambusi amesema kuwa tatizo kubwa linalowafanya timu ikose matokeo chanya ni kutokuwa na mawasiliano mazuri kwenye timu.


“Unajua tatizo ni kwamba wachezaji wanaocheza hatujazoea kuwaona. Kikosi kizima kimechanganywa kile.
Kuna hadi wapya waliosajiliwa juzi tunaona wanaingizwa kwenye kikosi cha kwanza.

 

Sasa hapo unakuta wachezaji hawajazoeana hata kidogo, hakuna uwiano mzuri kwenye timu, mawasiliano mazuri ya kwenye timu hakuna na ndiyo maana tunashindwa kupata matokeo mazuri hadi sasa.


“Kwa sababu ili kupata uwiano kwenye timu lazima wale watakaocheza pamoja angalau wawe na muda kidogo wa kukaa na kujuana vizuri ndani na nje ya uwanja, ili kupata ushindi leo lazima kicheza kikosi kamili,”alisema Mwambusi.

Stori na Manjiro Lyimo

DK MWAKA AFUNGUKA BAADA ya MANARA KUONDOKA, “SIMBA ITAMBUE THAMANI ya MANARA na KUIPA HESHIMA”…

Leave a Comment