
Rais Samia Suluhu Hassan, leo Agosti 16, 2021 anatarajiwa kuondoka jijini Dodoma kuelekea Malawi kwa ajili ya kushiriki mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika kuanzia Agosti 17 hadi Agosti 18, mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu, katika mkutano huo wa 41, pamoja na mambo mengine, wakuu wa nchi na serikali wa SADC wataithibitisha Malawi kuwa mwenyekiti wa SADC kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Agosti 2021 hadi Agosti 2022.
