×

Yanga Yaanza Mazoezi nchini Morocco – Picha

TIMU ya Yanga leo Agosti 17, 2021 imeanza mazoezi ya uwanjani kwa mara ya kwanza wakiwa nchini Morocco katika kambi yao ya maandalizi ya msimu mpya.

 

Yanga wamefanya mazoezi nje ya Uwanja Mkubwa wa mpira wa Grand de Marrakech wakiwa chini ya kocha wao mkuu Nesreddine Nabi akisaidiwa na kocha Mkenya Razack Siwa.

Eneo kubwa la mazoezi ya leo asubuhi yalikuwa maalum kwa ajili ya kufungua stamina na kuondoa uchovu wa safari ndefu ya masaa 12 waliyosafiri juzi kutoka jijini Dar es Salaam mpaka Morocco wakipitia Dubai.

 

Hakuna mchezaji aliyekosa mazoezi hayo kwa wachezaji ambao waliofika hapa kasoro wale ambao bado hawajafika hapa ambao ni beki Yannick Bangala na kiungo Khalid Aucho.

Leave a Comment