×

Idadi ya Waliofariki kwa Kimbunga Haiti Yafikia 2,189

IDADI ya watu waliokufa kutokana na tetemeko la ardhi nchini Haiti imefikia 2,189, hadi sasa shirika la kuwalinda raia la Haiti, limeripoti kuwa takriban watu 12,268 wamejeruhiwa kutokana na tetemeko hilo lililokuwa na ukubwa wa 7.2 katika kipimo cha Richta.

 

Hospitali zimefurika baada ya wagonjwa ambao walikuwa wameweka kambi nje kupelekwa ndani ili kuepukana na kimbunga, maelfu ya watu wamepoteza nyumba zao kutokana na tetemeko hilo la ardhi.

 

Maafisa wamewaonya wakaazi kuwa waangalifu na majengo yaliyopata nyufa kutokana na tetemeko hilo la ardhi na ambayo yanaweza kuanguka kutokana na mvua hizo.

 

Kituo cha taifa kinachoshughulikia vimbunga nchini Marekani, kimeonya kuhusu mafuriko na maporomoko ya udongo wakati ambapo kimbunga Grace kilichosababisha mvua kubwa kikiendelea kuikumba nchi hiyo.

Leave a Comment