
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA wamefariki dunia kutokana na ajali ya gari aina ya Landcruiser yenye nambari za Usajili STL 8825 Mali ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambalo liligonga Lori aina ya FUSO yenye nambari za usajili T 586 ANE.
Kaimu Meneja wa Forodha wa TRA wa Tunduma, Omary Mnzava amewataja watumishi watano wa mamlaka hiyo kikosi kazi cha fast track waliofariki ajalini leo asubuhi Jumatatu mkoani humo ni Azari Shifonike ambaye ni dereva, Joel Mitondwa, Saidi Buddy, Fahad Hassan na Benard Mashingi.
Ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Hanseketwa Wilayani Mbozi Mkoani Songwe majira ya saa 11 alfajiri leo Agosti 23,2021. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
