Mwenyekiti wa Mtaa wa Oysterbay, Mololo Abel Mwaisumo, amesema upekuzi uliofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi umebaini kuwepo kwa mali za raia wa China zinazotiliwa shaka.
Mwaisumo amesema mali hizo zimekamatwa na mamlaka husika kwa ajili ya uchunguzi, huku akieleza kuwa bado haijafahamika kwa undani mali hizo zinahusishwa na kosa gani.
Amesema uchunguzi unaendelea ili kubaini aina ya mali zilizokamatwa, umiliki wake pamoja na mazingira yaliyopelekea kukamatwa kwake.
Mwenyekiti huyo amewataka wananchi na wasamaria wema kuendelea kutoa taarifa kwa mamlaka husika pale wanapobaini au kulihisi jambo lolote linaloweza kuwa na viashiria vya ukiukwaji wa sheria.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa wananchi kushirikiana na vyombo vya dola kwa kutoa taarifa kwa wakati, ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa baada ya uchunguzi kukamilika.