
MEYA wa Jiji la Dara es salaam, Omary Kumbilamoto amefanya ziara kutembelea Ujenzi wa Barabara inayotoka Baracuda kuelekea Vingunguti Mataa. Mradi huo wa ujenzi wa Barabara hiyo upo katika hatua ya pili ya Ujenzi
Katika ziara hiyo Kumbilamoto kwa kushirikiana na Diwani wa Kata Liwiti Mhe. Alice waliweza kuzungumza na Wananchi ambao walikuwa wakikwamisha mradi huo kutokana na changamoto ya malipo ya fidia

Mhe. Kumbilamoto alifanikiwa kuzungumza na Wananchi hao na kukubaliana kupisha mradi huo ili uweze kuendelea kwa wakati na kiwango kinachotakiwa katika ziara hiyo Mh Meya alimshukuru Mh Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia bilioni 3 za ujenzi wa barabara hiyo mkandarasi ameahidi kukamilisha mwishoni mwa mwezi wa 9 na aliwapongeza Tarula kwa usimamizi mzuri wa barabara hiyo

Aidha Kumbilamoto alipokea kero za Maji hasa ya mvua na kumuagiza mkandarasa kuhakikisha ujenzi huwo wa Barabara kwa kiwango cha lami utatatua kero hiyo ya maji kwa kujenga mfereji ya maji.