
KWA kifupi tunaangalia mambo kumi ya kustaajabisha ya Tupac Shakur aliyefariki dunia Septemba 13, 1996 kwa kupigwa risasi huko Marekani.
Tupac alikuwa mwanamuziki mahiri wa Hip hop, rapa , mwigizaji, mtengeneza rekodi (record producer) mwanamashairi, mtunga filamu na mwanaharakati.
MOJA: Alipouawa, mwili wake uliteketezwa kwa moto (kwa mujibu wa tamaduni zao), cha ajabu wafuasi wake wa “outlaws” walichukua majivu yake, wakachanganya na bangi na kuvuta!
MBILI: Neno lake la mwisho kulisema kabla ya kifo chake ni neno “F*ck you!” alilomuambia askari aliyemuuliza ni nini kilikuwa kimemtokea.
TATU: Kinywaji alichokipenda zaid tupac kilikuwa Fanta orange. Alishawahi kuwafukuza badhi ya wafuasi wake nyumbani kwake kwa sababu eti walikuwa wanammalizia soda zake!
NNE: Akiwa mtoto mdogo akimkosea mama yake, alikuwa akipewa gazeti la New York Times alisome mbele ya mama yake!
TANO: Licha ya kuwa mwanafamilia nguli wa “West Coast”, cha kushangaza ni kwamba, Tupac alizaliwa New York ambako ni East Coast!
SITA: Alikuwa na uhusiano na msanii Madonna uhusiano ambao ulivunjika kutokana na Tupac kukashfiwa na watu weusi kwa kuwa na mpenzi mzungu!
SABA: Gazeti la Times, liliandika mahasimu wa Tupac, B.I.G na P.diddy walijua kuwa Tupac angeuawa wiki moja kabla madai ambayo yalikanushwa na FBI.
NANE: Aliandika wimbo wa Dear Mama akiwa jela. Mama yake alishawahi kufungwa jela pia!
TISA: Kwenye wimbo wake wa “Me and My Girlfriend” anachozungumzia ni bunduki yake na si mpenzi wake kama inavyojulikana.
KUMI: Alijaribu maisha ya jela kabla hajazaliwa kwani mama yake alifungwa akiwa na ujauzito wa wake.
Stori na Richard Manyota