The House of Favourite Newspapers

Mwanamke Mlinzi Avunjwa Mguu Akitoka Kazini-Video

0

Mwanamke mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, anayefanya kazi ya ulinzi katika kampuni binafsi ya ulinzi ya Kigeni, amegongwa na daladala na kusababisha mguu wake wa kushoto kuvunjika.

 

Katika tukio hilo lililotokea katika eneo la Mwananyamala A jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na waandishi wetu Richard Bukos na Issa Mnally, mlinzi huyo alikuwa akitembea kwa miguu kando ya barabara, ikielezwa kuwa alikuwa akirejea nyumbani kwake baada ya kumaliza lindo la usiku ambapo ghafla, ndipo daladala iliyopoteza mwelekeo ilipomvaa na kumgonga.

Leave A Reply