×

Majonzi: Vilio Vyatawala Kuagwa Kwa Mwili Wa Jackline Aliyefaliki Kwenye Ajali-Video

Basi la Kampuni ya Emigrace lenye namba za usajili T 703 DLG linalofanya safari zake kati ya Babati na Dar es Salaam, lilipata ajali katika mlima wa Kolo, Kata ya Kolo wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma.

 

Taarifa za awali kutoka eneo la tukio zilieleza kuwa, watu 9 wamepoteza maisha ambapo kati yao ni wanaume watu wazima wawili na mtoto mmoja wa kiume, wanawake wawili na watoto wawili wa kike na majeruhi zaidi ya 30. Mamia ya wakazi mjini Babati mkoani Manyara wajitokeza kuaga mwili wa Jackiline Mollel aliyefariki katika ajali ya gari iliyo waua watu 9 na kujeruhi wengine 40 katika milima ya kolo wilayani kondoa mkoani Dodoma.

Leave a Comment