×

Aishi na Kisu Tumboni kwa Miaka 3

David Mlilo mkazi wa nchini Zimbabwe amepanga kuishtaki hospitali ya Hippo Valley Medical Centre baada ya kugundua kuwa madaktari wa kituo hicho walisahau kisu tumboni mwake walipomfanyia upasuaji mwaka 2019.

Mlilo anataka fidia kutoka kutokana na kumsababishia matatizo makubwa ya kiafya, kiuchumi baada ya kupoteza ajira yake mwaka huu kutokana na ofisi yake kuchoshwa na kuumwa mara kwa mara.

Tatizo hilo aligundua baada ya kwenda katika hospitali ya Parirenyatwa iliyopo Harare na alipofanyiwa vipimo walibaini kuwa ana kisu tumbo, na sasa anaendelea na matibabu.

Leave a Comment