×

Rais Samia: Umeacha Mtoto Wajibika – Video

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewataka waliotelekeza watoto kuhakikisha wanawalea kwani ni wajibu wao na ni haki ya mtoto kupata matunzo na malezi ya mzazi wake.

 

Rais Samia amesema hayo leo Oktoba 6, 2021 wakati akihutubia kwenye uzinduzi wa Jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki katika eneo la National Capital City, Jijini Dodoma

 

“Naupongeza Mhimili wa Mahakama kwa kuanzisha vituo jumuishi mahususi vya kushughulikia masuala ya kifamilia, mirathi, talaka, ndoa, malezi na matunzo, hili ni jambo kubwa mno kwa sababu wanawake wengi na watoto wamekuwa wakiteseka.

 

“Nilipooneshwa chumba cha kunyonyesha nikampongeza Mtendaji Mkuu wa Mahakama kwamba mmefikiri vyema sababu ni kutokana na kutowajibika kwa wanaume ndiyo haya yametokea, wamejua kwamba kunataka kusikilizwa ndiyo maana wametenga vyumba.

 

“Somo kwa wanaume, sasa muwajibike, umeacha mtoto pahali wajibika, usijifiche, huyo ni kiumbe alikuja bila kutaka mwenyewe, ulimleta nenda kwawajibike, shirikiana na yule uliyeshirikiana naye kumleta duniani,” amesema Rais Samia.

 

Leave a Comment