
Abiria waliokuwa wanasafiri kutoka Mpanda mkoani Katavi kwenda Kasulu mkoani Kigoma, wamenusurika kifo baada ya Basi la Kampuni ya Adventure lenye namba za usajili T 186 AKX walilokuwa wakisafiria, kupinduka katika eneo la Mlima Kamba karibu na Mto Malagarasi, takribani Kilometa 2 kutoka Uvinza.

Ajali hiyo imetokea leo, Oktoba 18, 2021 majira ya saa nne asubuhi ambapo Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Uvinza, Mrisho Hassan amesema wamepokea majeruhi 16 ambao kati yao wanaume ni sita na wanawake 10.

Ameongeza kuwa majeruhi wanne kati yao, hali zao sio nzuri akiwemo kondakta wa basi hilo, Iddy Mande ambaye amekatika miguu yote na kusababisha apoteze damu nyingi na kuongeza kuwa hakuna taarifa za kifo huku jitihada za kumsafirisha kondakta huyo kwenda Hospitali ya Mkoa kwa matibabu zaidi zikifanyika.