
WAFANYABIASHARA wadogo (Machinga) zaidi ya 5,000 waliopo katika eneo la Makoroboi jijini Mwanza licha ya kutii agizo la Mkuu wa Mkoa huo Mhandisi Robert Gabriel la kuwataka kupisha katika eneo hilo wamemlilia Rais Samia kwani wamevunja vibanda vyao na hawana eneo mbadala la kufanyia biashara zao.
Machinga hao ambao walioamua kutii agizo hilo huku wakisema hawajui wapi wanaelekea baada ya maeneo waliyopangiwa kujaa, kilio chao wanakielekeza kwa Rais Samia Suluhu Hassan.
Hapo jana Mkuu wa Mkoa huo Mhandisi Robert Gabriel jana Oktoba 22, 2021, alitoa muda wa saa 24 kwa wafanyabiashara ndogo ndogo wa eneo hilo kuondoka na kwenda kwenye maeneo rasmi waliyotengewa.