×

Taliban Wataka Serikali Yao Kutambuliwa Kimataifa

KUNDI la Taliban Oktoba 30, 2021 wameomba Serikali yao kutambuliwa Kimataifa na kupewa misaada na Marekani na Mataifa mengine ya Magharibi ambayo yamewawekea vikwazo huku wakisema wanahitaji sana misaada ya kibinadamu kutokana na wananchi wake kukumbwa na njaa na hali mbaya ya kimaisha.

 

Hakuna Nchi ambayo imeitambua rasmi Serikali ya Afghanistan tangu ichukue Madaraka Mwezi Agosti. Taifa hilo linakabiliwa na majanga ya kiuchumi na kibinadamu.

 

Msemaji wa Taliban, Zabihullah Mujahid amesema kuendelea kutoitambua Serikali yao na kutowapa misaada kunaathiri maisha ya Raia wasio na hatia nchini humo na hili linaweza kuathiri sio tu Nchi hiyo bali Dunia nzima.

 

“Ujumbe wetu kwa Marekani ni kwamba kutoendelea kututambua kunasababisha matatizo kuendelea Afighanistan hili linaweza kuonekana ni tatizo letu tu lakini baadaye linaweza kuwa tatizo la Dunia nzima” amesema Msemaji wa Taliban.

Leave a Comment