×

Inspekta Mahita Kizimbani Ushahidi Kesi ya Mbowe

IKIWA ni muendelezo wa kesi namba 16/2021 ya Uhujumu Uchumi na makosa ya kupanga njama za kupanga kutekeleza matukio ugaidi na kufadhiri ugaidi, inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu hatimaye shahid wa 7 upande wa Jamhuri amewasili mahakamani leo Novemba 5, 2021 kwa ajili ya kutoa ushahidi wake.

 

Shahidi wa saba aliyejitambulisha kama Mkaguzi wa Jeshi la Polisi, Omary Mahita ambaye anafanya kazi Idara ya Upelelezi, mwenye umri wa miaka 36 akiongozwa na Wakili wa Serikali, Pius Hilla ameieleza mahakama namna alivyohusika katika tukio la ukamataji wa watuhumiwa watatu wanaotuhumiwa katika kesi hiyo.

 

Akitoa ushahidi wake mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu, Joachim Tiganga, Inspekta Mahita amesema alipewa maelekezo ya kuunda kikosi maalum ili kukitia nguvuni kikundi cha watu (watuhumiwa ambao ni Mbowe na wenzake, Halfan Bwire, Mohamed Ling’wenya na Adam Kasekwa maarufu kama Adamoo ) ambacho amedai kilikuwa kinataka kufanya vitendo vya kigaidi maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Mwanza, Arusha, Kilimanjaro na Mbeya.

 

Ametaja vitendo hivyo vya kihalifu ni kuchoma vituo vya mafuta, kuzuia barabara, kukata miti, kufanya maandamano yasiyo na kikomo pamoja na kumdhuru aliyekuwa mkuu wa wilaya ya hai kwa Kipindi hicho Lengai Ole Sabaya. Mpaka sasa, Inspekta Mahita bado yuko kizimbani anaendelea kutoa ushahidi wake.

 

SEHEMU YA USHAIDI HUO

Jaji: Majina yako

Shahidi: Inspector Mahita Mohamed

Jaji: Umri

Shahidi: 36

Jaji: Kabila

Shahidi: Mluguru

Jaji: Kazi

Shahidi: Askari Polisi

Jaji: Dini

Shahidi: muislam

Shahidi: Wallah wabillah watallah, Nathibitisha Kutoa Ushahidi Wa Kweli

Wakili wa Serikali: Ataongozwa na Wakili Pius Hilla

Wakili wa Serikali: Mahita Wewe ni Mkazi wa wapi

Shahidi: Mkazi wa Morogoro

Wakili wa Serikali: Tangu lini

Shahidi: Mwezi 04 Mwaka 2021

Wakili wa Serikali: Kabla Mwezi wa Nne ulikuwa Ukiishi wapi

Shahidi: Arusha

Wakili wa Serikali: Kazi yako ni Ipi

Shahidi: Polisi

Wakili wa Serikali: Tangu lini

Shahidi: Mwezi wa 03 2011

Wakili wa Serikali: Upo Kitengo gani

Shahidi: Idara ya Polisi Upelelezi wa Jinai

WS: Kwa Muda gani

Shahidi: Kwa Miaka 08

WS: Arusha Ulikwenda Lini

Shahidi: Tangu Mwaka 2014

WS: Mwaka 2020 ulikuwa kituo gani

Shahidi: Central Police Arusha

WS: Ulikuwa na nafasi gani

Shahidi: Msaidizi wa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Arusha

WS: Ieleze Mahakama ukiwa Kama Afisa wa Polisi Majukumu Yako yalikuwa ni yapi

Shahidi: Ukamataji wa wahalifu, Upekuzi wa tuhumiwa na Maeneo, Kusafirisha Watuhumiwa

WS: Unamaanisha Nini

Shahidi: Kuwatoa Watuhumiwa kuwatoa na kuwapeleka Sehemu Nyingine

WS: Kingine

Shahidi: Kuzuia na Kupambama na Uhalifu

WS: Kingine

Shahidi: Uandishi Wa Maelezo, ya Mashahidi na Watuhumiwa pamoja na Upelelezi wa Makosa ya Jinai

Kusimamia Askari waliopo Chini yangu

WS: Tarehe 04 August 2020 nini Kilotokea

Shahidi: Nikiwa Ofisini Arusha Nilipogiwa Simu na Afande Wangu ACP Ramadhan Kingai, aliniita Ofisini kwake

Aliniagiza Kutafuta Askari Wawili

Ambapo niliwatafuta Detective Francis na koplo Goodluck

Tulienda Ofisi ya Afande RCO akatuambia tunatoka Kwa ajili ya Safari ya kazi

Kuna kazi ya kwenda Kufanya

Wakili wa Serikali: Ilikuwa Majira ya Saa ngapi

Shahidi: Saa 11

Wakili wa Serikali: Kingai alisema mnapenda Kufanya kazi wapi

Shahidi: Tunaenda Kufanya kazi Moshi

WS: Ukiwa pale sasa na Goodluck pamoja na Francis kitu gani kilifuata

Shahidi: Tulijiandaa na Safari pamoja na Askari Mwingine anayetokea Ofisini Kwake

ASP Jumanne alikuwa na Yeye anatusubiria pale tujiunge naye kwa Pamoja twende Moshi

Alikuwa anatusubiria Arumeru

Wakili wa Serikali: Baada ya Kufika Arumeru Mlielekea Wapi

Shahidi: Tukiingiza Ofisi ya Polisi OC CID Arumeru, Mimi Afande Kingai, ASP Jumanne, PC GOODLUCK na PC Francis ili Kupata Briefing Ya kazi tunayo kwenda Kufanya

Shahidi: Tukiingiza Ofisi ya Polisi OC CID Arumeru, Mimi Afande Kingai, ASP Jumanne, PC GOODLUCK na PC Francis ili Kupata Briefing Ya kazi tunayo kwenda Kufanya

WS: Nani aliye fanya Briefing Siku hiyo

Shahidi: Afande Kingai ambaye ndiye alikuwa Kiongozi wetu wa Msafara

Wakili wa Serikali: Kwenye Briefing Mlielezwa Mambo gani

Shahidi: Afande Kingai alituambia Kuwa amepewa Maelekezo ya Kuunda Kikosi Maalum, na Kikosi Hilo Ndiyo

MIMI, ASP Jumanne, Goodluck, Francis, na PC Aziz

Kwamba Kuna Kikundi Cha Watu kinataka Kufanya Vitendo Vya kigaidi

WS: Vitendo gani hivyo

Shahidi: Kuwa Kikundi hicho kinataka Kufanya Vitendo Vya Kigaidi Mikoa Mbalimbali ikiwemo Arusha, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Mwanza na Mbeya

Uhalifu walipokuwa wanataka Kufanya ni KUCHOMA Vituo Vya Mafuta, Kuzuia Barabara, Kukata Miti, kuwadhuru Viongozi

Wa Serikali Ikiwemo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Hai, Ole Lengai Sabaya

Maandamano ambayo haya Ukomo, na Pia alitueleza Washirika ambao wanataka Kufanya Matukio hayo

WS: Aliwataja akina nani

Shahidi: Afande Kingai alisema Mpango huo ulikuwa unaratibiwa na Mheshimiwa Freeman Mbowe.

 

Kwa taariza zaid ya kinacheondelea kujiri mahakamani katika kesi ya Freeman Mbowe, Dar es Salaam na ileya Lengai Ole Sabaya kule Arusha, tufuatilie katika tovuti yetu na Instagram page yetu ya GlobalPublishers.

Leave a Comment