×

Shigongo Ataka Mnong’ono wa Taifa – Video

 

MBUNGE wa Buchosa, Mhe. Eric Shigongo ameishauri Serikali kuwa na ajenda tekelezi ya kitaifa ya kuwawezesha vijana wazawa ili kujiendeleza na kujikwamua kimaisha tofauti na sasa hivi ambapo vijana wengi wanamaliza masomo yao ya juu na kukosa cha kufanya kutokana na kukosa vipato wezeshi.

 

“Nasikitika kwamba vijana wetu hatuwapi kipaumbele kwenye suala la maendeleo ya taifa lao. Tunawapeleka shule wanasoma wanapata elimu lakini wakija mtaani hawana cha kufanya.

 

“Ninapenda kushauri tuanzishe MFUKO WA UBUNIFU WA TAIFA ili uwasaidie vijana wabunifu wanapomaliza masomoyao na kutengeneza bidhaa mbalimbali ambazo zitangia sokoni.

 

“Hatuwezi kuwa na vijana ambao wamesoma, wana elimu lakini haisaidii kufanya maendeleo kwa taifa letu. Ninaomba tuwe na MNONG’ONO WA TAIFA. Hatuwezi kunong’ona kama taifa kwamba fedha zote za tenda ziende kwa vijana wazawa badala ya kuwapa wazungu? Au kama wanakuja wazungu wafanya pamoja na vijana wazawa ili kuwajengea ujuzi na sehemu ya pesa hiyo ibaki kwa vijana wetu?

 

“Barabara ya Buchosa – Sengerema ikajengwe na mzawa, mzunguko wa pesa utabaki kwa vijana wetu, baada ya miaka kadhaa tutakuwa na mabilionea wengi.

 

“Tusipofanya hivyo watu watakuja hapa na mabegi wanaondoka wakiwa matajiri wakati vijana wetu wakibaki na chuki na hatutatengeneza mabilionea wapya.

 

“Wakati umefika kwa vijana wa nchi hii kunufaika na utajiri wa Taifa lao. Afika Kusini waliweza, sisi Tanzania tunashindwa nini?”, amehoji Shigongo.

 

Leave a Comment