×

Vanessa Apigwa Tukio Kama Zuchu

MWANAMAMA aliyetundika daruga kunako Bongo Fleva, Vanessa Mdee au V-Money anawatahadharisha wasanii Bongo juu ya kukubali kutumika vibaya na kupigwa matukio na makampuni ambayo yanataka kuendeleza maslahi yao kwa kutumia umaarufu wa wasanii hao.

 

Vanessa anasimulia jinsi benki moja maarufu ilikosa kumlipa hata baada ya yeye kutangazwa kuwa balozi wa benki hiyo.

Vanessa ambaye anajulikana kwa ngoma zake kali kama Niroge, anafichua kuwa japo benki aliyoihudumia ilikuwa bora hadi sasa wamekaa kimya na hawatimiza makubaliano waliokuwa nayo ya malipo.

 

Vanessa anawashauri wasanii kuwa makini wanapofanya biashara na makampuni. Ujumbe wa Vanessa unakuja wiki kadhaa baada ya msanii Zuchu pia kulalamika kuhusu makampuni kutowalipa wasanii hasa wa kike.

Leave a Comment