×

Rick Ross Kwenye Mahusiano Mapya


Rapa na muanzilishi wa Lebo ya Maybach Music Group, Rick Ross anausishwa kutoka kimapenzi na comedian na rapa mwenzake, Vena Excell almaarufu Pretty Vee kufuatia ukaribu waliokuwa nao wawili hao.

Siku za hivi karibuni, Rick Ross aliusishwa kutoka kimapenzi na mwanamitindo kutoka Tanzania, Hamisa Mobetto baada ya kusambaa kwa vipande vya video na picha zikiwaonesha wawili hao wakila bata la kufa mtu, Dubai.

Taarifa zinaeleza, Rapa Rick Ross alimsaini Pretty Vee mapema mwaka huu katika lebo yake ya Maybach Music huku akimuaidi mrembo huyo kumsaidia kukua kimuziki, na sasa inaonekana kama wawili hao wamefikia hatua ya kuwa wapenzi.

Cc; @bakarimahundu

Leave a Comment