
Manchester City itazindua sanamu ya Sergio Leonel Agüero del Castillo, maarufu kama Kun Agüero nje ya Uwanja wa Etihad mwaka 2022, ikisimama pamoja na Vincent Kompany na David Silva.
Aguero ambaye ni raia wa Argentina alijiunga na Manchester City Julai 28, 2011 akitokea klabu ya Atletico Madrid ya Hispania, amecheza City kwa mafanikio makubwa.
Nyota huyo amelazimika kutangaza kustaafu rasmi mchezo Soka baada ya kupatwa na tatizo la moyo.
Vilabu na wachezaji mbalimbali wameungana kumtakia kheri nyota huyo kwa kumtumia salamu mbalimbali za upendo.