Airtel na Letshego Wawajaza Mkwanja Washindi wa Kuza Akiba na Ushinde Droo ya 4
WATEJA wa Benki ya Letshego na Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel, leo Jumatano wameondoka na mkwanja kiulainiii baada ya kuibuka kidedea kwenye promosheni ya Kuza Akiba na Ushinde ambapo droo ya nne ilichezeshwa na jumla ya washindi 25 waliondoka na mkwanja.
Akizungumza kwenye hafla ya kuchezesha droo hiyo, Meneja Matukio wa Aitel, Dangio Kaniki amesema hiyo ni promosheni ya tatu ambapo wameendelea kumwaga mkwanja wa wateja wao wakishirikiana na Benki ya Letshego.
Dangio amewashauri watumiaji wengine wa simu za mkononi kutumia mtandao wa Airtel na kushiriki kwenye promosheni hiyo ambapo mshindi katika droo ya mwisho anatarajiwa kujizolea kitita cha shilingi milioni tano.
Katika droo hiyo washindi 25 walipatikana ambapo walipigiwa simu na kukabidhiwa pesa hiyo papo hapo.
Kwa upande wake Meneja Masoko wa Benki ya Letshego, Uswege Mwaipyana amesema benki yake inaendelea kushirikiana na Airtel kumwaga mapesa kwa ajili ya washindi wa promosheni hiyo.
Uswege amewataka wateja wa Aitel na Letshego kuendelea kushiriki promosheni hiyo ambapo droo ya mwisho ina zawadi kubwa tatu ambapo mshindi wa kwanza ataondoka na pesa taslimu milioni tano, wa pili milioni mbili na nusu na wa tatu ataondoka na milioni moja. HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS/ GPL