×

Rais Samia Awalilia Waliokufa Maji Zanzibar

Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi kufuatia vifo vya watu 10 waliofariki dunia katika ajali ya boti iliyotokea Januari 4, 2022 katika eneo la Bahari la Kisiwa cha Panza, Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba, Zanzibar.

 

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu, Rais Samia amemuomba Rais Dkt. Mwinyi kufikisha salamu za pole kwa wafiwa wote, ndugu, jamaa pamoja na marafiki na anaungana na familia hizo katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na kuwaombea marehemu kwa Mungu aziweke roho zao mahali pema peponi.

 

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kusini Pemba, Richard Mchomvu, watu hao walikuwa wanatoka Chakechake kuelekeakwenye mazishi katika Kisiwa cha Panza, Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba.

Leave a Comment