×

Diamond: Nitaandika historia mpya Dar Live

Funga Mwaka Concert 2015 (10)
Diamond akiwasalimia mashabiki wake, juzi katika  eneo la Karume, Ilala jijini Dar.

Musa Mateja

ZIKIWA zimesalia saa kadhaa kufika Sikukuu ya Krismasi ambapo ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar kutakuwa na burudani kabambe, staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, amesema kuwa siku hiyo ataandika historia mpya.

Akizungumza na waandishi wa habari eneo la Karume, Ilala jijini Dar, Diamond ambaye siku hiyo ataongozana na madansa wake kutoa burudani mwanzo mwisho, huku akiimba nyimbo zake zote ‘live’ kwa kutumia vyombo, alisema hana budi kufurahi na mashabiki wake kwa kuwa MTV Africa Music Awards (MAMA) waliamua kumpa tuzo ya Mtumbuizaji Bora wa Mwaka.
DIAMOND (2)
“Nawaomba tu mashabiki wangu wote mje kwa wingi, naahidi sitawaangusha kwa namna yoyote ile maana hakuna kitu ninachojitahidi kwenye maisha yangu kila kukicha kama kutowaudhi, njooni tuandike historia mpya ya pamoja Dar Live,” alisema Diamond.

Mkutano huo maalum ulihusisha waandishi wa habari na wapenzi wa muziki wa Bongo Fleva huku lengo kuu likiwa ni kuzungumzia shoo hiyo kubwa kuliko zote kwa mwaka huu, ambapo imepewa jina la Funga Mwaka Concert.

Funga Mwaka Concert 2015 (20)Pia waandaji wakuu wa shoo hiyo, Global Publishers Ltd, kupitia kwa Meneja Mkuu, Abdallah Mrisho, naye alizungumza machache pamoja na kutambulisha listi ya wasanii wengine watakaoambatana na Diamond siku hiyo.

“Mbali na Diamond pia tutakuwa na Msagasumu, Wakali Dancers, Staric pamoja na burudani nyingine nyingi. Haitakuwa shoo ndogo, Diamond ameamua kufurahi na mashabiki wa muziki siku ya Krismasi kwa kufunga na kuukaribisha mwaka mpya 2016. Shoo zitaanza asubuhi kwa watoto mpaka saa 12 jioni kisha baada ya hapo ni watu wazima mpaka alfajiri,” alisema Mrisho.

Funga Mwaka Concert 2015 (19)…akigawa CD za nyimbo zake kwa mashabiki.

Kwa mujibu wa mratibu wa shoo hiyo, Juma Mbizo, viingilio katika shoo hiyo ni Sh. 15,000 kawaida na kwa V.I.P ni Sh. 30,000.

Wadhamini wakuu wa shoo hiyo, Mtandao wa Simu za Mkononi wa Airtel, kupitia kwa Afisa Uhusiano, Jenny Matinde wao wametoa ofa ya punguzo la bei kwa tiketi 1,000 za awali kwa watakaokata kupitia kadi mpya za Airtel Tap Tap zenye mfumo mpya wa kulipia bili mbalimbali.

“Kadi za Tap Tap zinazorahisisha kufanya malipo zaidi popote ulipo bila ya gharama yoyote tayari zinapatikana maeneo ya Temeke na Ilala lakini kuwa nayo unapaswa kuwa na kadi ya Airtel na kwa wateja 1,000 wa kwanza wenye Tap Tap watakaokata tiketi kupitia kadi hizo, watakuwa na punguzo la Sh. 5,000 yaani kwa 15,000 itakuwa 10,000 na 30,000 itakuwa 25,000,” alisema,” Matinde.

Pia usiku huo kutakuwa na zawadi kwa mshindi wa Shindano la Ijumaa Sexiest Girl ambapo hadi sasa wamebaki washiriki watatu walioingia fainali ambao ni Asha Salum ‘Kidoa’, Elizabeth Michael ‘Lulu’ pamoja na Vanessa Mdee ‘Vee Money’.

Leave a Comment