
MWISHO wa reli Kigoma? Ndivyo unavyoweza kujiuliza kufuatia kile kinachoonekana sasa mara baada ya Rayvanny kumu-unfollow mpenzi wake, Paula Kajala kunako Instagram pamoja na kufuta picha zote walizowahi kupiga pamoja.
Pia Paula ambaye anaripotiwa kurejea Bongo akitokea masomoni nchini Uturuki, naye amefanya kitu kama hicho kwa Rayvanny.
Penzi la wawili hao lilichipuka kwenye uso wa dunia mara baada ya Rayvanny kuachana na mzazi mwenzake, Fahyma.
Kama utakumbuka miezi minne iliyopita, Rayvanny aliachia video ya wimbo wake, Wanaweweseka ambapo Paula alitokea kama video vixen, lakini za ndani kabisa zinasema penzi lao linapumulia mashine.