Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiagana na Wazee wa Zanzibar waliofika katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Karume kabla ya kuondoka na kuelekea nchini Ufaransa leo 09 Februari, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Februari 9, 2022 ameondoka kuelekea Nchini Ufaransa na baadaye Ubelgiji kikazi. Akiwa Ufaransa, atahudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali utakaojadili kuhusu Rasilimali Bahari Duniani
Aidha, atashuhudia utiaji saini baina ya Serikali ya Tanzania na Ufaransa katika Sekta za Miradi ya Maendeleo, ushirikiano katika masuala ya Uchumi wa Buluu, Usalama wa Bahari, Sekta ya Usafiri na Maendeleo Endelevu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango pamoja na Rais wa Zanzibar Mhe. Husein Ali Mwinyi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Karume Zanzibar kabla ya kuondoka kuelekea Nchini Ufaransa leo tarehe 09 Februari, 2022.