
Taarifa ya Baraza la Famasi imesema Baraza hilo limekuwa likifuatilia mwenendo wa utoaji wa dawa za macho kwenye baadhi ya maduka ya dawa Nchini ambapo limebaini utoaji holela wa dawa za matone za macho zenye viambata vya antibiotic na steroid kwa Wagonjwa wa Macho Mekundu (RedEyes) wanaofika kupatiwa huduma kwenye baadhi ya maduka hayo
Kufuatia mwenendo huo Baraza limewataka watoa huduma wote kwenye maduka ya dawa kuacha mara moja kutoa dawa ambazo sio rasmi kwa ajili ya matibabu ya Macho Mekundu na ambazo hazijaandikwa na daktari, na kuwaelekeza Wananchi kwenda kupata matibabu kwenye Vituo vya Afya vyenye Wataalamu wa Macho
Aidha Wananchi wametakiwa kuacha kujinunulia na kutumia dawa kiholela kutibu ugonjwa huo kwani dawa hizo za macho zinaweza kusababisha madhara ikiwemo upofu endapo zitatumika bila ushauri wa daktari