×

Zungu Achaguliwa Kuwa Naibu Spika

WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wamempitisha Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu kuwa Naibu Spika wa Bunge hilo leo Ijumaa, Februari, 11, 2022.
Wabunge waliopiga kura – 301
Kura za NDIO – 296 (98.33%)
Kura za HAPANA -3
Kura Zilizoharibika -2.
“Nichukue nafasi hii kwa niaba yenu wote wabunge kumpongeza Mhe Zungu kwa ushindi wa kishindo wa kuwa msaidizi wangu, nampongeza kwa sababu yale makofi yaliyokuwa yanapigwa wakati akija hapa yameonekana dhahiri kwenye kura nyingi mlizompa,” amesema Spika, Dkt. Tulia Ackson.

Leave a Comment