×

Waziri wa Afya Zanzibar Apokea Mashine za Oxygen.

 

Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui amepokea mashine tatu za kufua oxygen zenye thamani ya Tsh. Millioni 14 kutoka kwa @dorismollelfoundation kwa kushirikiana na @segalfoundation mashine hizi ni kwa ajili ya kusaidia vitengi vya watoto njiti katika Hospitali ya Fuoni iliyoko Magharibi B, Unguja, Zanzibar.

Vifaa hivi vilipokelewa katika hafla fupi iliyofanyika katika Hospitali ya Fuoni na kuhudhuriwa na Viongozi kutoka Wizara ya Afya, Ofisi ya Mrajis wa Mashirika yasiyo ya kiserikali, viongozi kutoka @segalfoundation wakiongozwa na Mkurugenzi wa Programs Bi. Gladys Onyango pamoja na wadau wa Afya, Zanzibar.

Leave a Comment